Hadithi Kutoka Ulimwenguni Pote

Mara kwa mara tunapokea ushuhuda kutoka kwa wachungaji, viongozi wa makanisa na waamini kutoka ulimwenguni kote kutokana na mafundisho ya Derek Prince. Gundua kwa nini huduma ya Derek Prince imekuwa chanzo cha kuaminika cha mafundisho ya Biblia tangu 1971.

Watu Wanasema Nini

Niliongozwa kwa mafundisho ya Derek Prince miezi michache iliyopita. Siwezi kumshukuru vya kutosha kwa kila kitu nilichojifunza. Ulimwengu mpya wa maarifa ya kiroho umefunguka kwangu. Namsikiliza kila siku na namshukuru Baba wetu wa Mbinguni kwa mafundisho yake.

Carmen M, Ufaransa

Nimekuwa nikimtazama Derek Prince kwenye YouTube kwa miaka kadhaa sasa. Mafundisho yake ni thabiti na yanaburudisha kiasi kwamba hata sasa yanaendelea kuleta mabadiliko wakati ambapo mafundisho thabiti ni adimu.

Minerva O, Marekani

Nimejifunza mengi kutoka kwa mafundisho yenu.

Mchungaji Lazarous P, Zambia

Nimekuwa nikisikiliza mafundisho ya Derek Prince na yamebadilisha maisha yangu. Asante huduma ya Derek Prince.

Susannah T, Australia

Maisha yangu yamebadilishwa na mafundisho ya Derek Prince.

Miriam G, Uingereza

Ninaendelea kubarikiwa na kuhamasishwa na huduma ya Derek Prince! Asante kwa kufanya mafundisho ya Derek kupatikana kwa urahisi.

Lynne C, Marekani

Ninapenda huduma hii. Nilifunguliwa kutoka katika minyororo ya adui.

Patrice A, Trinidad na Tobago

Kwa bahati nilikutana na mojawapo ya mafundisho ya Derek Prince kwenye YouTube. Katika dunia tunasema 'kwa bahati', lakini najua hii haikuwa bahati. Ninaamini kweli kuwa hii ilikuwa ni Roho Mtakatifu akiniongoza na kunielekeza katika kweli zote. Na hili lilianza takriban mwezi mmoja uliopita na nimekuwa nikitazama kila siku.

Lisa J, Marekani

Nimebarikiwa sana na Huduma ya Derek Prince . Mafundisho yake yako wazi na mimi ni msikilizaji wa mara kwa mara.

Darryl L, Marekani

Nilipata mahubiri ya Derek Prince wakati wa kufungiwa ndani kutokana na janga na nimekuwa nikihisi amani na furaha nikiwa nasikiliza mafundisho yake.

Meing, Malaysia

Nilibatizwa nikiwa sekondari na nilijihusisha sana na Ukristo, lakini sikujua kazi ya Kristo msalabani ilikuwa kwa ajili yangu. Nilifikiri Yesu alikuwa anahitajika na wengine, lakini sio mimi. Niliishi maisha ya dhambi. Miaka kadhaa baadaye nilichoshwa na maisha yangu yaliyo tupu na nilitaka mwelekeo thabiti. Nilitazama video zote za kutia moyo nilizoweza kupata lakini hakukuwa na amani ya kudumu ndani yangu. Baada ya muda wa kutafuta, niliamua kumtafuta Mungu kwa dhati. Usiku mmoja niliinama kwenye chumba changu na kumuomba Mungu anisamehe, kisha nikaanza kusoma Biblia tena. Mungu alinielekeza kwa Warumi 10:9-10 na akanipa imani ya kuikubali. Hatimaye nilijua Yesu Kristo alifanya nini kwa ajili yangu msalabani. Sifa kwa Mungu! Kupitia YouTube, nimepata mafundisho mengi ambayo yameimarisha imani yangu, na yanafaa sana katika uhusiano wangu na Kristo.

Samuel Z, Taiwan

Maisha yangu kamwe hayatakuwa vilevile baada ya kusikiliza mafundisho ya Derek Prince. Imekuwa miezi miwili sasa na nimejitolea kabisa katika uhusiano wangu na Mungu, mazungumzo yangu na mawazo yangu. Utukufu kwa Mungu! Asante.

Shawnda J, Marekani

Derek Prince ndiye mwalimu wangu. Ninajifunza kutoka kwake kila siku. Amekuwa baraka maishani mwangu na namshukuru Bwana wetu kwa hili. Asante!

Carmen R M, Ufaransa

Asante kwa huduma yenu ya kudumu kwa ulimwengu. Nimekuwa nikisikiliza mafundisho ya Derek Prince wakati mwingi mwaka uliopita. Ni msukumo mkubwa.

Daniel, Uingereza

Miaka michache iliyopita nilikuwa nikitafuta kwa hamu mtu wa kunifundisha Neno la Mungu. Hadi wakati huo, sikuwa nimepata yeyote na maarifa yangu yalitokana na kusoma tu. Wakati huo nilikuwa nikimtafuta Mungu na nilikuwa napitia YouTube, ambapo nilipata mafundisho kutoka kwa Derek Prince. Nilivutiwa sana. Tangu wakati huo, nimekuwa nikitazama video zake kila siku.

Bruno S, Ureno

Derek Prince alinifungua macho kupitia mafundisho yake na akaniwekea mfano wa kufuata.

Lucinda, Marekani

Mimi na mke wangu tuligundua mafundisho ya Derek kwenye YouTube na yalitusaidia sana kuelewa vita vya kiroho. Sasa tumekombolewa na tunaendelea kutembea kwa imani na Yesu.

Pietro P, Uswisi

Namshukuru Mungu kwa huduma ya Derek Prince . Mko mahali sahihi kwa wakati sahihi.

Charles M, Marekani

Nilizaliwa katika familia ya Kihindu lakini nilimkubali Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wangu miaka michache iliyopita. Tangu wakati huo, niligundua Derek Prince kwenye YouTube na nimeponywa msongo wa mawazo. Nimejifunza mengi na nimepata mwalimu wa Biblia anayeaminika (baada ya kutafuta kwa muda mrefu). Asante sana huduma ya Derek Prince kwa kueneza Neno la Mungu na Injili kote ulimwenguni.

Shreyas J, India

Leo ilikuwa ni siku yangu ya kwanza kutazama ujumbe wa Derek Prince. Ulinifanya nishawishike sana. Asante.

Theresa, Marekani

Nimebarikiwa sana na mafundisho ya Derek Prince.

Annamma Q, India

Namshukuru Mungu kwa Derek Prince Ministries. Ni baraka kuwa na mafundisho kama haya yaliyo ya kina na yanayogusa moyo.

Ann M P, Marekani

Hapo awali nilikuwa najaribu kusoma Biblia lakini sikuielewa kwa sababu nilikuwa na tafsiri King James. Sikuwa najua kuwa kulikuwa na tafsiri zingine. Sikujua kabisa. Kwa hiyo nilijaribu kutafuta kanisa la kwenda kwa sababu nilifikiri bila shaka nitaelimishwa na wataelezea. Nilienda katika makanisa kadhaa na mwishowe nilikatishwa tamaa. Hakuna mtu karibu nami aliyeweza kunionyesha njia. Kwa hiyo nilikata tamaa! Hivi majuzi nilikuwa nikitazama YouTube na nikakutana na Derek Prince. Sasa namsikiliza kila siku! Alikuwa mtu niliyekuwa nikimtafuta. Ninamshukuru sana kwamba video zake bado ziko na zinatafsiriwa. Ninajifunza sana! Natazama video zake kila siku.

Belisa G, Marekani

Nimetiwa moyo sana na ujumbe wa Derek Prince Ministries. Shauku yangu imeongezeka kujifunza Neno la Mungu na kuleta baraka katika familia yetu. Asanteni kwa rasilimali zote mlizoweka.

Pilli B, India

Mafundisho ya Derek Prince yamebadilisha maisha yangu. Sasa ninaishi nikiwa na ufahamu zaidi kuhusu ulimwengu wa rohoni kuliko hapo awali. Nimefurahi kuwa katika safari hii mpya na Roho Mtakatifu. Kujifunza kuhusu laana na baraka kumepangwa na Mungu. Hata kupitia ujumbe wa video za mtandaoni za Derek Prince, ninahisi uwepo wenye nguvu wa Mungu ndani ya chumba changu. Nabii wa kweli na mtumishi wa Mungu. Nangojea kumsalimia na kumshukuru mbinguni!

Suzie Grace, Muungano wa Falme za Kiarabu

Namshukuru Derek Prince kwa mafundisho yake ya kina! Upendo wake, uvumilivu, na kujitolea kulionekana wazi tangu mwanzo! Alinifundisha sana! Yeye ni mmoja wa wahubiri wangu wa kutegemea! Mungu alizungumza kupitia kwake na alinisaidia kufungua macho yangu kwa ukweli!

Elizabeth, Kanada

Derek Prince