Yaliyomo
(Bonyeza ili kusogea mahali)
- Derek Prince alizaliwa wapi?
- Derek Prince alizaliwa lini?
- Derek Prince alifariki?
- Derek Prince alifariki akiwa na umri gani?
- Derek Prince alifariki akiwa wapi?
- Derek Prince alizikwa wapi?
- Derek Prince alifariki vipi?
- Derek Prince aliamini nini?
- Tafsiri gani ya Biblia Derek aliipenda zaidi?
- Derek Prince alikuwa ameoa?
- Lydia Prince alifariki lini?
- Ruth Prince alifariki lini?
- Derek Prince alikuwa na watoto?
Derek Prince alizaliwa wapi?
Bangalore, India.
Derek Prince alizaliwa lini?
14 Agosti 1915
Derek Prince alifariki?
Derek Prince alifariki tarehe 24 Septemba 2003.
Derek Prince alifariki akiwa na umri gani?
Miaka 88 (1915-2003)
Derek Prince alifariki akiwa wapi?
Derek Prince alifariki nyumbani kwake huko Yerusalemu.
Derek Prince alizikwa wapi?
Makaburi ya Kimataifa ya Kanisa la Alliance, Yerusalemu.
Derek Prince alifariki vipi?
Derek Prince alifariki usingizini kutokana na matatizo ya moyo baada ya kipindi kirefu cha afya kuzorota.
Derek Prince aliamini nini?
Derek Prince alikuwa Mkristo wa Kipentekoste asiyeegemea dhehebu lolote wala kikundi chochote. Imani zake zinakubaliana na Tamko letu la Imani linalotuongoza katika masuala yote ya imani na matendo.
Tamko la Imani“Wakati mwingine watu wanaponiuliza, ‘Wewe ni wa dhehebu gani, unahudhuria kanisa lipi?’ Napenda kujibu, kama Mwandishi wa Zaburi: ‘Mimi ni rafiki wa wote wanaomcha Mungu, wote wanaofuata maagizo yake.’ Sio sana kuhusu jina la dhehebu; ni suala la mtazamo wa moyo na mwelekeo wa maisha.” - Derek Prince
Tafsiri gani ya Biblia Derek aliipenda zaidi?
Derek alipendelea Tafsiri ya King James na hata alisoma maandiko ya awali ya Kiebrania na Kigiriki.
Ili kuwasiliana vyema na wasikilizaji, mara nyingi alitumia tafsiri za kisasa kama vile New American Standard Bible, New International Version na New King James Version. Wakati mwingine alirejelea Biblia ya J.B. Phillips, The Living Bible au Amplified Bible, ikiwa ilielezea vizuri kifungu na maana yake.
Derek Prince alikuwa ameoa?
“Nilikuwa nimeoa Lydia kwa miaka 30 na Ruth kwa miaka 20. Na ndoa zote mbili zilikuwa zenye furaha na mafanikio.” - Derek Prince
Lydia Prince alifariki lini?
Oktoba 5 1975 (akiwa na umri wa miaka 85)
Ruth Prince alifariki lini?
Desemba 29 1998 (akiwa na umri wa miaka 68)
Derek Prince alikuwa na watoto?
Derek Prince alikuwa baba wa watoto 12.